DIAMOND AWAFUNGA MIDOMO WANAOSEMA NILLAN SIO MTOTO WAKE

• Apost picha na kuandika ujumbe unaoonyesha Prince Nillan ni damu yake


Star kutoka Bongo, Diamond Platnumz amewafunga midomo wale waliokuwa wakisema mtoto wake wa pili aliyezaa na mpenzi wake Zari sio wa kwake bali ni wa mume wa zamani wa Zari, marehemu Ivan.
Kupitia page yake ya Instagram Mond amepost picha akiwa amewapakata watoto wake wote wawili, Latifa a.k.a Tiffah pamoja na Nillan na kuandika ujumbe ambao unaonyesha wazi kuwa Nillan ni mtoto wake na sio vile watu wanavyoongea.
Mara nyingi katika mitandao ya kijamii watu wamekuwa wakipost kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond na kupost picha wakimfananisha na mume wa zamani wa Zari ambaye kwa sasa ni marehemu na alijulikana kwa
jina la Ivan Don.

“ My sperms and I!!!!” ameandika Diamond.

Please follow and like us:

HARMONIZE KUSEPA WCB

• Afunguka tetesi za yeye kuhama WCB

Mwanamuziki anayetokea katika label ya WCB inayomilikiwa na ‘Diamond Platnumz’ ‘Harmonize’ ambaye kwa sasa anabamba na ngoma yake ya ‘Shulala’ aliyofanya collabo na msanii kutoka Nigeria ‘Korede Bello’ amesema WCB ni kama mzazi kwake hivyo sio rahisi yeye kuondoka katika label hiyo.
Harmonize amesema WCB imemtoa mbali na inamlipa sana hivyo yeye hana ndoto hiyo ya kuondoka katika label hiyo.
“Hapana kwasababu unapomzungumzia Harmonize unaizungumzia WCB ,so bila WCB hakuna Harmonize ,yaani kama baba kama mama” amesema Harmonize

Please follow and like us:

AUNT EZEKIEL AFANYA KUFULU

• Ni katika birthday yake

Mwanadada muigizaji wa bongo movie ‘Aunt Ezekiel ‘ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na dancer wa ‘Diamond Platnumz ‘ ‘Mose Iyobo’‘Cookie’ amefanya party kubwa katika kumbukumbu yake yakuzaliwa .

Katika sherehe yake iliyofanyika October 27 katika ukumbi wa kifahari Masaki jijini Dar es salaam “Rodizio ‘ ameonekana ametumia pesa nyingi kutokana na hadhi ya hotel yenyewe na hata hivyo alipata ushirikiano wakutosha kwani waigizaji wenzake hawakumtupa
Aunt Ezekiel ameonekana kuwa more happy katika sherehe yake huku akienjoy na wasanii mbalimbali.

Please follow and like us:

AMBER LULU NA PREZZO WAZIDI KUTUPA VIONJO

• Penzi lao lazidi kunoga mtandaoni

Mwanadada ambaye ni msanii pia ni video vixen ‘Amber Lulu ‘ na anayesemekana kuwa ni mpenzi wake wa sasa’Prezzo’ wamezidi kuchafua mtandao wa Instagram licha ya Prezoo kukana kuwa hawana mahusiano .
Kupitia page yake ya Instagram mwanadada ‘Amber Lulu’ amepost picha akiwa yeye na Prezzo ikimuonesha Amber ameshikwa makaliona msanii huyo kutoka Kenya.

“Achana na picha link kwenye bio hapo juu” aliandika Amber Lulu

Please follow and like us:

RUBY AFUNGUKA COLABO YAKE NA YEMI ALADE

• Amesema mambo yakiiva tutajua

Mwanadada ambaye ni msanii wa Bongo Fleva ‘Ruby’ amefunguka tetesi za ujio wa colabo yake na msanii wa Nigeria ‘Yemi Alade’.

Ruby amesema hawezi weka wazi swala hilo kwani yeye mambo ya nje na nyumbani huwa siri sana kwake na kama ipo ikiwa tayari tutajua tu.
“siwezi nikasema tayari kila kitu kimemalizika lakini vitu vipo ,sitaki kusema kabisa kwenu kolabo za kimataifa natamani iwe surprise kwasababu nimekaa muda mrefu kimya I need talk to about home kwanza “amesema Ruby

Please follow and like us:

WANAHABARI WAKAMATWA!

Ni huko Nay Pyi Taw katika mji wa Burma baada ya kurusha drone juu ya jengo la bunge

Mamalaka ya Mynmar inawashikilia wanahabari wawili wa kigeni kwa kosa la kurusha ndege ndogo yenye camera, siku ya ijumaa.
Wakala wan chi ya Myanmar ameripoti kuwa wanahabari hao wawili ambao mmoja anatokea Sngapore na mwingine Malaysia, wapo chini ya ulinzi mkali baada ya drones hizo kuonekana zikirushwa kutokea upande wao.
Wizara ya ndani ya imekaririwa ikisema kuwa wawili hao wametambuliwa kama wafanyakazi wa Turkish Radio na Television Corporation (TRT).

Ripoti imesema wawili hao walikuwa na lengo la kupiga picha jingo la Bunge la Nay Pyi Taw na tayari mamlaka ya nchi hioimeutaarifu ubalozi wa Singapore na Malaysia ili kufahamu dhumuni la wanahabari hao.

Please follow and like us:

SETH WA IPTL YUPO HATARINI

• Ni baada ya tupo lililopo tumboni mwake kuisha muda wake


Upande wa utetezi katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Sethi na mwenzake, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa puto lililowekwa tumboni kwa Sethi limeisha muda wake na lisipobadilishwa litamsababishia kifo.
Wakili wa Sethi, Alex Balomi alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mshitakiwa huyo alipelekwa kufanyiwa vipimo Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini hadi leo hajapatiwa majibu yake ya vipimo wala kupatiwa matibabu.
“Lengo la Mahakama hii kutoa amri ya kumpeleka mshitakiwa kupata matibabu lakini hakupata majibu ya vipimo ambazo ni taarifa zake binafsi. Mteja wetu ana wasiwasi kwa kuwa hajapewa majibu ya vipimo alivyochukuliwa kwa sababu ya athari ya puto lililowekwa tumboni,”alisema Balomi.
Hata hivyo, Wakili Balomi alidai mshitakiwa amewalalamikia kuwa hajapata majibu yoyote baada ya vipimo na ndio maana ana hofu. Hakimu Shaidi alisema Mahakama ilitoa amri kwamba Sethi apelekwe hospitali na amepelekwa, hivyo daktari amekamilisha kazi yake na kwamba mawakili wanaweza kwenda kuulizia kuhusu vipimo vyake.

Please follow and like us:

MAGUFULI AFUNGUKA MIKOPO YA WANAFUNZI

• Amedai kuwa atashangaa sana kuona fedha alizoidhinisha kwa ajili ya mikopo hazitawafikia walengwa kwa wakati


Rais Dkt Magufuli amesema mwezi uliopita Wizara ya Fedha na Mipango ilitoa Sh bilioni 147 zilizoidhinisha kwenda Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaostahili kupata.
“Nitashangaa sana kama patakuwepo wanafunzi waliopo kwenye orodha ya kupata mikopo na wawe hawajapata, nitashangaa sana kwa sababu mimi najua nimeshaidhinisha fedha hizo na zimeshatoka,” alisema Rais Magufuli.
Alisema kuwa ameyasema hayo kwa sababu inaweza kutokea wanafunzi wakafungua vyuo na kuanza kuhangaika vyuoni bila kupata mikopo, jambo ambalo hataki kulisikia.
“Ndiyo maana wakati mwingine nalazimika kuwaza kuwa fedha zimewekwa benki kwenye fixed deposit (akaunti ya muda maalumu) zinamzalishia mtu,” alisema Rais Magufuli.

Please follow and like us: