TWITTER KUFIKIA MANENO 280


Mtandao maarufu Duniani Twitter ambao una watumiaji zaidi ya milioni mia tatu, umekuwa ukikabiliwa na changamoto za ukuaji na hivyo kuamua kutafuta namna mbalimbali za kukuza wigo wa watumiaji kwa mtandao huo.
Mtandao huo umetangaza jaribio lake la kuongeza idadi ya maneno ya ujumbe ambayo mtu anaweza kuandika kwenye mtandao huo kwa mara moja hadi kufikia 280 ambayo ni mara mbili ya kiwango cha idadi ya maneno yaliyopo kwa sasa.
Kwenye Kampuni hiyo ya Twitter, jaribio hilo la kuongeza zaidi maneno ni moja kati ya hatua za kutatua moja ya changamoto iliyokuwa ikiwasumbua watumiaji wengi wa mtandao huo.

Please follow and like us:

DUDU BAYA NA MANENO MAZITO KWA MWANAYE


Msanii mkongwe wa Bongo Flavor Dudu Baya ameshusha maneno mazito kwa mwanae Wille baada ya kudai kukataa shule.
Akipiga stori na Bongo five amesema,
“Mungu mwenyewe alisema mtoto mwenye busara na hekima humfurahisha babaye lakini na toto jinga, shenzi na pumbavu ni mzigo kwa mama,” Dudu Baya ameiambia Bongo5.
“Mara nyingi watoto wa namna hii, vibaka, wezi, chagudoa, mashoga wanakaaga sana na mama zao lakini baba yoyote mtoto wa namna hiyo hawezi kukaa naye, huwa wanaitimua ndio maana mtoto anaweza kuwa kibaka mwizi akapelekwa jela baba yake asiende kumuangali lakini mama yake akaenda,” Dudu Baya ameongeza kuwa sasa hatamtafuta mwanae huyo kwani ni kijana mkubwa mwenye umri wa kati ya miaka 16 hadi 17.

Please follow and like us:

MBUNGE KUKOJOA HADHARANI


Ibrahim Abiriga mbunge kutoka Uganda amekiri kuwa alikojoa hadharani katika uzio wa Wizara ya Fedha baada ya kubanwa na mkojo. Wakati akifanya mahojiano na kituo cha runinga cha NBS Abiriga alisema “jana nilikuwa nimebanwa sana, nikaenda kukojoa”Abiriga.
Alipoulizwa na mwandishi wa habari kwanini alifanya vile, mbunge huyo alijibu kwa mshangao akiuliza kwa nini asifanye hivo, kwanini abane mkojo?
Mbali na tukio hilo I brahim Abiriga ni miongoni mwa wabunge wanaounga mkono kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa umri wa raisi ambapo katiba ya Kenya hairuhusu mtu anayegombea Uraisi kuwa na umri zaidi ya miaka75.

Please follow and like us:

CR7 AFIKISHA MECHI 400 MADRID

Hapo jana wakati timu ya Real Madrid ikiivaa Dortmund ya Ujerumani katika ligi ya mabigwa wa ulaya, mchezaji Christian Ronaldo amefanikiwa kuichezea timu hiyo mechi 400 tangu ametua katika timu hiyo akitokea Manchester United na tayari Ronaldo ameichezea timu ya Real Madrid mechi za La Liga 267.
Pamoja na hayo gwiji la Real Madrid Raul Gonzalez ndiye anaeshikilia nafasi ya kwanza kwa kuichezea timu hiyo mechi 741 katika michuano yote, hii ni tangu kuanzishwa kwa Real Madrid ambayo ni moja ya klabu kongwe ulaya na duniani kote ambapo ni wachezaji 22 tu walioweza kufikisha mechi 400.
Baada ya beki Mbrazil, Roberto Carlos aliyefanikiwa kucheza mechi 527 na beki mwingine Mbrazil ambaye bado anacheza, Marcelo aliyefikisha mechi 416, kwa sasa Ronaldo anakuwa mchezaji wa tatu mgeni kucheza mechi nyingi za real Madrid.

Please follow and like us:

Majukumu ya Tambwe kuchukuliwa na Chirwa

http://1.bp.blogspot.com/-PcQv0Bxa480/VQ52GN53dXI/AAAAAAABfLY/0hRwe0k4nvk/s1600/TAMBWE.jpg

       Kutokana na Tambwe kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha la goti na kumsababishia kukosa mechi tano ambazo Yanga imecheza ikiwepo mchezo wa ngao ya jamii na minne ya ligi kuu Bara Kocha mkuu wa Yanga amemkabidhi Obrey Chirwa majukumu ya Mshambuliaji Amissi Tambwe.

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema kukosekana kwa Tambwe hakuna tatizo lolote kwani Chirwa yupo na atabeba majukumu yote ya Tambwe kwa muda huu ambao mchezaji anauguza goti lake.

“Ninachokifanya ni kwamba, kwenye kikosi changu natengeneza ile hali ya kwamba akikosekana mmoja basi anakuwepo mwingine wa kuziba pengo lake”alisema Lwandamila.

Please follow and like us:

Myweather aongeza mjengo

 

https://i.ytimg.com/vi/TgphavF2qwo/maxresdefault.jpg

       Baada ya kumchapa McGregor katika raundi ya 10,inadaiwa bondia Myweather alilamba Zaidi ya pauni millioni 250 (Tsh bilioni 752), ambapo kwa sasa bondia huyo amenunua jumba lenye thamani ya bilioni 56 katika eneo la watu wazito la Beverly Hills.

Bondia huyo mmarekani ambaye hajawahi kupigwa katika pambano lolote kati ya 50 aliyocheza anaendelea kufurahia maisha ya kustaafu baada ya kumchapa bondia Muirishi, Conor McGregor jijini Las Vegas.

Jumba hilo jipya alilonunua lina vyumba sita vya kulala na mabafu kumi, pia lina chumba maalum cha sinema ambacho kinaweza kuchukua watu 50 na likiwa na vinywaji, chocolate na pipi.

Myweather amecheza ngumi kwa miaka 21 na alistaafu Agost 26 akiwa ameingiza fedha nyingi Zaidi ya bondia yeyote kihistoria,Mmarekani huyo anadai kuwa yeye ndiye bondia wa kwanza kuingiza Zaidi ya dola bilioni moja katika mchezo huo mgumu Zaidi.

Ikumbukwe kuwa Myweather ana jumba jingine Las Vegas na linguine Miami ambalo lina thamani ya pauni milioni 5.69(Zaidi ya shilingi 17).

Please follow and like us:

Ben Pol:Napenda mwanamke mwenye confidence.

https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2017/05/ben-pol-1.png

Siku chache baada ya aliyekuwa anadaiwa kutoka kimapenzi na Ben Pol ambaye ni msanii wa vichekesho Anastazia Kizaveli ‘Ebitoke’ kulalamika kwamba hapokelewi simu yake wala kujibiwa ujumbe mfupi na Ben Pol, hatimaye Pol amefunguka kuhusu sifa za mwanamke anayempenda.

Ben Pol amesema sifa pekee anayoangalia kwa mwanamke anayeweza kumpenda ni lazima awe anajiamibi pindi akiwa anaongea naye.

“Endapo nikimpenda msichana sifa kubwa ni confidence yake pindi tunapoongea au kuchat,U-Smart na uharaka katika kujibu vitu anavyoulizwa kwa wakati huo”amesema Ben Pol.

Please follow and like us:

IDADI YA WANAOSUBIRI KUNYONGWA YAONGEZEKA TANZANIA.

https://iranhr.net/media/content/images/noose54.jpg.885x520_q85_box-0%2C0%2C884%2C520_crop_detail_upscale.jpg

Ripoti iliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika mafunzo kwa waandishi wa habari mjini Morogoro hivi karibuni, ilibainisha kuwa hakuna hukumu yoyote ya kifo iliyosainiwa na Rais ili kutekelezwa kutoka mwaka 1994 hadi Oktoba 2015. Na hivyo ripoti hii kupelekea idadi ya wanaosubiri kunyongwa kuongezeka na kufikia 467.

Baada ya mahakama kuu ya Sumbawanga mkoani Rukwa, kuwahukumu watu wawili wakazi wa kijiji cha kaengesa wilayani Sumbawanga kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke na kumsababishia kifo, imepelekea idadi hiyo kuongezeka na mahabasu 465 wakiwemo wananwake 20 na wanaume 445 kusubiri adhabu hiyo.Ripoti hii ni kutoka (UPR) mpango wa kujitathmini kuhusu hali ya utekelezaji wa haki za binadamu.

Please follow and like us: