BEN POL KUPATA DILI UFARANSA

• Ni baada ya kulamba shavu la ubalozi wa taasisi inayojihusisha na mambo ya afya kwa watoto Nchini Ufaransa

Msanii wa muziki wa R&B ndani ya Industry ya Bongo Benard Paul aka Ben Pol amefunguka issue ya kupata dili nchini Ufaransa akiwa kama balozi.
Be pol amedai kuwa katika hafla inayotarajia kufanyika mwezi huu atatangazwa kuwa balozi wa taasisi hiyo inayojishughulisha na kusaidia watoto katika mambo ya Afya
“Nipo mjini Paris (France) kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya MAUA Association ,itakayofanyika tarehe 18 Novemba 2017 mjini humu,hafla hiyo itaambatana na utambulisho rasmi wa Ben Pol kama balozi mpya wa MAUA Association kwani ni taasisi iliyoundwa na kusajiliwa nchini Ufaransa kwa minajili ya kutoa usaidizi wa kiafya kwa watoto na vijana ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao@feelingood@feelingloved@godbless “Amesema Ben Pol.

Please follow and like us:

NUH AKANA KUIMBA NA ALIYEMCHUKULIA MKE

• Hii ni baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anafahamiana na mwanaume huyo na wameshafanya wimbo pamoja


Baada ya habari kusambaa katika mitandao ya kijamii kuwa mawanaume aliyemuoa aliyekuwa mke wa Nuh Mziwanda kwamba aliwahi kufanya naye kazi na ndiye aliyemtoa kijijini kwa Iringa.
Nuh amekana taarifa hizo na kudai kuwa hamfahamu mwanaume huyo kama watu wanavyodai kuwa alimtoa Iringa na kuja kukaa naye ambapo ndipo alipofahamiana na mke wake.
“ Simfahamu kabisa huyo mwanaume zaidi ya kumuona kwenye picha, nawaomba mashabiki wangu wasinihusishe kabisa na hao watu maana kama ni Nawal yupo na maisha yake na mimi nipo na maisha yangu, nipo kikazi zaidi kwani kwa sasa ninatembea mikoa mbalimbali kufanya show wala sina habari na mtu” alisema Nuh Mziwanda

Please follow and like us:

SONIA AFUNGUKA NA KUWATAJA WALIOCHANGIA KUHARIBU SOKO LA BONGO MOVIE

• Amesema kuwa ni producers na baadhi ya wasanii pia aomba serikali kuingilia kati suala hilo


Muigizaji mkongwe wa movie za kibongo Farida Sabu amabaye wengi humwita Sonia amefunguka issue kibao ikiwemo kuyumba kwa soko la filamu za kibongo kwa sasa.
Kupitia mahojiano yake na See The African Movie amewatupia lawama baadhi ya waigizaji mastaa ambao walifanya kazi ya uandaaji na usambazaji,
“hii tasnia imeangushwa kwa mabo mengi sana, tumekuwa tukiitupia sana serikali lawama, wakati tunaanza filamu zilikuwa zinawalipa sana producers na sio sisi waigizaji, kiukweli walitengeneza pesa nzuri sana kupitia sisi, amabpo sisi tulikuwa tunalipwa kidogo na ndipo wasanii wakubwa waliokuwa na uwezo kuamua kufanya kazi zao wenyewe” amesema Sonia.
Pia akiongea kuhusu uwezekano wa kuirudisha Bongo movie ya zamani Sonia amedai kuwa inawezekana pale ambapo wataanza kutegemeana na serikali sio kusimama msanii kama msanii kwani uwezo huo hawana.

Please follow and like us:

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI 30 MATATANI

• Watakiwa kutoa maelezo kwa kushindwa kuwawezesha maofisa maendeleo jamii kufika katika mkutano wa 12 wa kujadili maendeleo ya jamii

Katika mkutano huo wa kikazi wa maofisa hao, halmashauri zilizopeleka wajumbe ni 30 tu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Selemani Jafo alisema kitendo cha wakurugenzi hao kinazuia nia njema ya Serikali ya kusukuma maendeleo kwa wananchi wake.
Alisema maofisa hao wana kazi nyingi za maendeleo ya wananchi na kutowawezesha katika mkutano ni kuwanyima maarifa mapya ya kazi na hasa kubadilishana uzoefu kati yao. Alisema serikali inawategemea maofisa hao kufanikisha miradi ya maendeleo hasa ile ya elimu na ufahamu kuzuia mitafaruku maeneo yao na kuhamasisha maendeleo ya jamii.
“Wananchi wana matarajio makubwa na serikali na mabadiliko hayawezi kuja bila kuwa na mabadiliko katika utendaji kazi,” alisema. Alisema kutokana na wajibu wao, serikali sasa inapiga marufuku maofisa hao kusimamia miradi ya Tasaf na Ukimwi pekee bali waandae mikakati ya kuwawezesha wananchi kutambua fursa na kutekeleza miradi ya maendeleo yao.
Waziri Jafo aliwataka maofisa maendeleo ya jamii kufanya kazi ya kupiga vita maovu katika jamii ikiwamo mauaji ya vikongwe na albino. Ofisa Maendeleo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam Mwajuma Magwizu kwa niaba ya wenzake alisema watatekeleza maagizo waliyopewa kwa ufasaha ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

Please follow and like us:

ATUPWA JELA MIAKA MITATU

• Ni baada ya kukutwa na hatia ya utapeli wa ajira kwa watu 144


Kapeele Mpundililwa ambaye ni mkurugenzi wa shirika la umoja wa watu wa Afrika (APAPO), amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Katavi kwenda jela miaka mitatu.
Kapeele alipatikana na hatia hiyo baada ya kuwatapeli watu 144 kuwa angewaajiri katika shirika hilo na ndipo Hakimu Odira Amworo alitoa hukumu hiyo jana mjini hapa baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa pasipo kutia shaka yoyote.
Hakimu Amwolo alieleza kuwa miongoni mwa ushahidi uliomtia hatiani mshitakiwa ni hati za waliotapeliwa ajira alizolipia kwenye benki, akaunti iliyokuwa ikimilikiwa na mshitakiwa mwenyewe ambazo ziliwasilishwa mahakamani kama kielelezo huku zikiwa na majina ya wote waliotapeliwa.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alifanikiwa kuwatapeli watu 144 ambao wote walilipa jumla ya Sh milioni 3.9 ikiwa ni ada ili waweze kusailiwa na kuajiriwa na shirika hilo.

Please follow and like us:

FAIZA ALLY NA VICHUPI

• Adai kuwa hakuna kitu ambacho ana-enjoy kama kutembea nusu utupu


Ex girlfriend wa Mbunge wa Mbeya Mh Joseph Mbilinyi, Faiza Ally ambaye amekuwa ni mrembo asiyekaukiwa na vituko hasa katika social medias amezidi kuja na mapya.
Faiza ameibuka na kudai kuwa anaamini kuwa siku moja atafanikiwa kumpata mwanaume ambaye atakuwa pia anapendelea style yake ya uvaaji wa nusu utupu.


“I hope siku moja nitapata mume atakae elewa chupi zangu, tukaishi maisha flani hivi amazing, maana sina mpango wa kuacha chupi kwa kweli na hivi nina mpango wa kuwa tajiri ndio kabisa maana sitarajii kuajiriwa ni chupi mwanzo mwisho acha niwe bibi bomba ndio maisha yangu ninayo yapenda, japo yana ni cost lakini kama kuna kitu na enjoy ni kutembea nusu uchi, YES!” aeandika Faiza katika ukurasa wake wa Instagram.

Please follow and like us:

TAHIYA AMUOMBA THE BOSS LADY MSAMAHA

• Ni kutokana na video yake iliyoleta utata akiwa na Diamond Platnumz


Mwanamitindo na mtangazaji Tahiya J. George aka Life of Tahiya amefunguka na kuomba radhi kwa Zari kuhusiana na issue hiyo.
Kupitia Dizzim Online mrembo huyo amesema kuwa


“Diamond is a very nice person, ni mtu ambaye yupo confortable sana ukiwa naye karibu, so nadhani he is a family guy, na kutokana na hilo wala sijapata shida yoyote na Zari, na ktu cha kwanza watu inabidi wajue kuwa ninamheshimu sana Zari na ninawaheshimu wote wakiwa kama mke na mume, na kama Zari aliichukulia vibaya ile situation, basi I apologise because I never meant anything bad to happen” amesema Tahiya.

Please follow and like us:

HAKUNA WA KUNILINGANISHA NA AKINA AMBER LULU

• Adai mkwanja anaolipwa kwenye video queen unamtosha kabisaaa!


Msanii anayekuja kwa kasi hivi sasa, Pretty Kindy amedai kuwa kwa video queen ambao wametimkia katika muziki akiwemo Amber Lulu, hakuna wa kumlinganisha nao.
Pretty amesema kuwa hawezi kukimbia kuwa video queen kama walivyofanya wakina Amber Lulu na Gigy Money na wengine kwa sababu anajiamini na analipwa vizuri na hata kwenye muziki bado hajaona wa kumpa changamoto.
“ Kiukweli hakuna wa kunilinganisha na hao wengine, juzikati nilikula dili la uvideo queen kwenye ngoma ya Benny Kinyaiya na nililipwa vizuri sana, lakini siwezi kuikimbia tasnia hiyo, kisa malipo, maana kama ni fedha ninajua nitalipwa za kutosha” alisema mwana dada huyo.

Please follow and like us: