MIMI MARS SIJAKOPI MELODY YA VANESSA

 

  • Ni kutokana na madai ya melody ya dede kuwa amecopy kwenye wimbo wa Vanessa wa duasi

 

Msanii wa muziki Bongo, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sitamani’, Mimi Mars amefunguka ishu ya kukopi melody kutoka Vanessa Mdee.

Mimi amedai kuwa si kweli ngoma yake ‘Dedee’ amechukua melody kutoka kwenye ngoma ya Vanessa na Legendury Beatz  ‘Duasi’ ila ni watu kusindwa kutofautisha

“Sijui labda zinafanana lakini nahisi kila mmoja ana njia yake, unaweza kukuta kitu kidogo tu ukasema hii kama ya wimbo ule lakini hiyo ipo hata kwenye muziki wa nje” Amesema Mimi Mars.

Please follow and like us:

JAY DEE : ASLAY NI MOTO WAKUOTEA MBALI

 

  • Amesema mziki wa aslay unamvutia anaweza kusikiliza hata siku nzima

     Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa ‘I miss you’ Judith Wambura aka Lady Jay Dee amefunguka kukunwa kwake na kazi za msanii mwenzake Aslay Isihaka aka Aslay anazozifanya kwa sasa

     Jide amesema anapohitaji kusikiliza muziki mzuri ,husikiliza nyimbo za Aslay na amekuwa akiusikiliza hata kutwa nzima kwa kuwa kazi zake zinakata kiu ya burudani anayoitaka

“mimi ni mwimbaji ,lakini haina maana kwamba sipati burudani kwa wenzangu ,mfano huwa natumia saa nyingi ,wakati mwingine nashinda kutwa nzima nasikiliza kazi za aslay ,anajua kuimba na kuandika nyimbo nzuri “amesema jaydee

Please follow and like us:

JIKE SHUPA NA SKENDO YA MASHOGA

 

  • Amefunguka tetesi zinazoendelea za kuuza watu wanaojishughulisha na mapenzi ya jinsia moja

     Mwanadada ambaye ni video vixen Bongo Zena Abdallah aka Jike Shupa amefunguka skendo inayomkabili kwa sasa ya kuwauza wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kusema kuwa hajihusishi na hajawahi fanya

     Jike Shupa amesema kuwa muda mrefu amekuwa akisemwa kuhusika kuwatafutia mabwana wanaume mashoga ,kitu alichodai ni uongo bali ni kumchafulia tu

“Nina marafiki wengi wa kiume ,labda miongoni mwao kuna wanaojihusisha na vitendo vya kishoga ,ila mimi sihusiki kwa kuwatafutia watu hao mabwana ,wanaozungumza hivyo wana nia ya kunichafua “Amesema Jike Shupa

Please follow and like us:

PIGO KWA MREMBO IRENE UWOYA

• Ni baada ya kuondokewa na aliyekuwa mume wake wa zamani Ndikumana

Mume wa zamani wa mrembo anayefanya poa katika Bongo movies Irene Uwoya, Ndikumana Hamad Katauti amabye pia alikuwa ni kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda amefariki dunia.
Uongozi wa timu hiyo umesema jana Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya lakini mwili wake umekutwa nyumbani kwake mjini Kigali akiwa amefariki dunia.
Mpaka sasa bado haijajulikana kifo chake kimesababishwa na nini kwani hakuwa mgonjwa na wala hajafanya ajali. Mwili wake umepelekwa monchwari ya kiislamu ya dispensari ya Rwampala kwa maombi ya familia yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram marehemu Ndikumana alitupia ujumbe wa shukrani kwa mama yake juu ya kuchagua mwanamke atakayemfaa kuishi naye.

Please follow and like us:

KYLIE JENNER ACHUKIZWA NA BABY SHOWER YAKE

• Alitamani ifanyike katika club ya Los Angels inayo-trend sana lakini haikuwa hivyo


The last born kutoka katika familia maarufu nchini Marekani ya The Kardashians Kylie Jenner amechukizwa na almost kila kitu katika party yake ya Baby shower.
Mrembo huyo mwenye umri wa mika 20 ambaye anatarajia kupata mtoto with her boyfriend Trivis Scott alilazimika ku-held a boring party nyumbani kwake kama sehemu ya kuendeleza reality show yao ya Keeping Up with the Kardashians.


“ilikuwa ni pajama party katika bustani, marafiki wote walikuwa organized na ma-producer pamoja na mama yake aitwaye Kris. Kris ni producer kwahiyo alikuwa aki-manage episode ya kipindi cha KUWTK. Marafiki wa Kylie hawakuweza kutumi mitandao ndio maana picha hazikuvuja na kila mmoja alizuiwa ku-take selfies kwa ajili ya Snapchat just in case” alisema insider.
Boyfriend wa mrembo huyo pia hakufanikiwa kufika katika party hiyo kutokana na commitments za tour za kimuziki.

Please follow and like us:

SOUDY BROWN ATEMA CHECHE

• Ni baada ya mrembo mmoja kumlalamikia jamaa huyo kutumia lugha moja tu akiwa anagawa ubuyu

Mwandishi na mtangazaji machachari wa kipindi maarufu hapa town cha Shilawadu Soudy Brown ameibuka na kumwaga maneno heavy kwa mmoja wa shabiki wake.
Kupitia mtandao wa Instagram Soudy ametokwa na maneno hayo baada ya fan huyo kuandika kuwa,
“He! He! He! Soudy, kwahiyo pale ambapo ni matangazo ya biashara in London unaweka caption za kiingereza ili fans wako wa London waweze kukuelewa vizuri lakini ikiwa ni suala la umbeya basi unaweka caption za Kiswahili ili fans wako wa London wasikuelewe, sisi pia tunataka caption za kiingereza katika posts zako za gossip” ameandika fan huyo ambapo Soudy hakusita kuijibu kuwa,
“My dear, hukunilipia ada yangu ya shule, pili, kuandika ubuyu(umbeya) kwa kiingereza haunogi kwahiyo usinichoshe kuandika English, na tatu kiingereza huku kimekuja na Boti” ameandika Soudy.

Please follow and like us:

REKODI YAVUNJWA KATIKA MLIMA MREFU AFRICA

• Ni baada ya raia wa Hispania kufanikiwa kuvunja rekodi yakuupanda mlima huo kwa baiskeli

Mpanda milima mashuhuri duniani kwa kutumia Baiskeli, Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli kwa siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito na wenzake wawili, Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema, aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika
Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa za Kilimanjaro, Arusha na Saadani inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio vya utalii katika Hifadhi zake 16. Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anaeleza hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.

Please follow and like us:

RIDHIWANI KIKWETE AMPA TANO ALI KIBA

• Ni baada ya kushinda tuzo za AFRIMA nchini Nigeria

Usiku wa kuamkia leo tarehe 13, November wasanii kutoka Bongo Ali Kiba pamoja na Nandy walishinda tuzo za AFRIMA ambazo zilifanyika nchini Nigeria.
Kupitia page ya Instagram Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amempongeza Ali Kiba kwa kuileta tuzo hiyo nyumbani pamoja na kuishukuru management ya Ali Kiba.

“Congratulation to our Ali Kiba anda your management for bringing home the AFRIMA 2017 awards. You deserve them bro… Ushauri wangu kwako,,, keep that good music alive” ameandika Ridhiwani.

Please follow and like us: