ATUPWA JELA MIAKA MITATU

• Ni baada ya kukutwa na hatia ya utapeli wa ajira kwa watu 144


Kapeele Mpundililwa ambaye ni mkurugenzi wa shirika la umoja wa watu wa Afrika (APAPO), amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Katavi kwenda jela miaka mitatu.
Kapeele alipatikana na hatia hiyo baada ya kuwatapeli watu 144 kuwa angewaajiri katika shirika hilo na ndipo Hakimu Odira Amworo alitoa hukumu hiyo jana mjini hapa baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa pasipo kutia shaka yoyote.
Hakimu Amwolo alieleza kuwa miongoni mwa ushahidi uliomtia hatiani mshitakiwa ni hati za waliotapeliwa ajira alizolipia kwenye benki, akaunti iliyokuwa ikimilikiwa na mshitakiwa mwenyewe ambazo ziliwasilishwa mahakamani kama kielelezo huku zikiwa na majina ya wote waliotapeliwa.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alifanikiwa kuwatapeli watu 144 ambao wote walilipa jumla ya Sh milioni 3.9 ikiwa ni ada ili waweze kusailiwa na kuajiriwa na shirika hilo.

Please follow and like us:

Comments

comments