AMA KWELI ELIMU HAINA MWISHO

 

  • Hii ni baada ya baba wa watoto 14 akijiandaa kumaliza elimu ya msingi

         Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ambaye pia ni baba wa watoto 14 mkazi wa wilaya ya Kamuli, John Bosco Mutebe anajiandaa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Novemba, mwaka huu.

Mutebe mwenye umri wa miaka 44, ataungana na wanafunzi wenzake 128 wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kyeera, Kata ya Namwendwa kufanya mitihani.

Jumatano iliyopita, baba huyo wa mabinti 11 na watoto watatu wa kiume ambaye ni kiongozi Kanda ya Bwaguusa, alishiriki ibada maalumu ya kuombea wanafunzi wa darasa la saba iliyofanyika Kanisa Katoliki Namwendwa na kuongozwa na Padri Fredrick Wobeera.

“Ninaheshimika na nina uelewa mkubwa wa mambo, ndiyo maana ninashikilia ofisi ya umma, lakini siku zote nimekuwa nikijisikia vibaya kutokana na elimu duni,” alisema Mutebe anayeamini atafaulu na kuingia kidato cha kwanza mwakani akiapa kusoma kwa bidii na hatimaye awe mtaalamu wa kilimo kwa kuwa tayari ni mkulima na anapenda kilimo.

Please follow and like us:

Comments

comments