ALIYOJITABIRIA HAMISA YAMEMTOKEA

• Alitaka kuzaa na mwanaume maarufu ambaye tayari ana mwanamke mwingine

Waswahili husema lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja, hayo yamejidhihirisha kwa mwanamitindo maarufu hapa Bongo Hamisa Mobetto kuzaa na msanii mkubwa Diamond Platnumz ambapo inasemekana alijitabiria hayo katika movie inayoitwa ‘Poor Player’inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Moja kati ya watu waliopo katika filamu hiyo Seth Bosco amesema kuwa katika movie hiyo Hamisa amecheza kama mwanamke aliyzaa na mwanaume mwenye mwanamke mwingine kisha kumtelekeza kitu ambacho ndio kimemtokea sasa hivi.
“Yaani Mobeto ni kama alijitabiria mapema, maana kabla hajazaa alicheza filamu kama amezaa na mwanaume mwenye mwanamke mwingine kisha akamtelekeza na mtoto kitu ambacho kimemtokea kweli baada ya kuzaa na Mbongo Fleva na kumtelekeza kwa kutotoa matumizi ya mtoto,” alisema Seth.

Please follow and like us:

Comments

comments