ACHA NIKAE KIMYA HAWAKAWII KUNITIA LOCK UP

  • Unakataa goli halali, fowadi anamkimbia beki unasema kaotea! hii ndiyo ligi ya Bongo

 http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2017/04/20170419_120140.jpg

Afisa habari wa club ya Simba Haji Manara amewapa lawama waamuzi wa mchezo uliochezwa kati ya Simba dhidi ya Stand United kuwa walichokifanya siyo sahihi kwa kulikataa goli la wazi na kutoa penati yenye utata.

Kupitia ukurasa wake maalum wa Instagram Manara aliandika hayo baada ya kumalizika kwa mchezo ambapo Simba waliwaburuza Stand United kwa kuwachapa magoli 2-1 na kufikisha alama tatu za mchezo huo.

“Hii ndiyo ligi ya Bongo na hao ndio marefa wetu, unatoa penati tata kisha unakataa goli halali, fowadi anamkimbia beki unasema kaotea!. Acha nipige kimya hawakawii kunitia lock up” amesema Manara.

Kwa sasa Simba inaongoza ligi kuu Tanzania Bara kwa alama 11, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar pamoja na Azam FC kwa alama hiyo huku wakitofautiana idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga.

Please follow and like us:

Comments

comments